Kocha msaidizi wa Simba, Juma Mgunda, ameyakubali matusi aliyotukanwa na msemaji wa Yanga, Ali Kamwe na kusema kuwa kama amefanya hivyo ili timu hiyo ishinde kwenye mchezo wake wa kwanza wa fainali dhidi ya USM Alger ni sawa.
"Yanga ni klabu yetu pekee Tanzania inayotuwakilisha kwenye fainali hii ya CAF.
Na kwa bahati iliyo njema inacheza na klabu inayotoka nje ya nchi yetu.
Sijui kinachopelekea mimi kuwa miongoni mwa kampeni hii ya matusi na kunidhalilisha!
Nilidhani kampeni itakuwa ni kushinda fainali, kuliko hiki alichokifanya mwanangu, Ally Kamwe.
Namuombea kwa Mungu awe na mwisho mzuri, mimi nimeshuhudia watu wengi wakifanya kazi Yanga na Simba na sasa wapo nje ya mfumo.
Kama nilipaswa kutukanwa ili Yanga ishinde basi nimekubali ili Taifa langu lijivunie.
Tusiposhinda kesho nitashangaa sana kwanini tumefungwa wakati kilichotakiwa kifanywe kimefanywa juu yangu na familia yangu."
0 Comments