Ticker

7/recent/ticker-posts

HALI ZA WALIONUSURIKA KWENYE AJALI YA NDEGE 192 5H-FZS BADO SI NZURI

Manusura wa ajali ya ndege 192 5H-FZS iliyotekea leo katika kiwanja cha Matambwe kilicchopo kwenye kiwanja cha Hifadhi ya Taifa ya Nyerere leo Mei 18,2023 saa tano na nusu asubuhi, hali zao bado si nzuri. 

Taarifa ya ajali hiyo imeweka wazi kuwa majira ya saa tano na nusu asubuhi ndege aina ya cessina 192 5H-FZS ikiwa na abiria watatau (3) na rubani 1 jumla 4 ambao majina yao ni Kapteni Benard Shayo - FZS, Aman mgogolo FZS, SCR Theonas Mnota na CRIII Evanda Elisha) wakiwa wanaenda doria kwa kutumia ndege hiyo, walipata ajali wakati ndege hiyo ikiruka katika kiwanja cha ndege Matambwe.

Kutokana na ajali hiyo, watu wawili ambao ni Kapteni Bernard Shayo na Amani Mgogolo walifariki dunia . 

Askari wawili walijeruhiwa na hali zao sio nzuri.

Baada ya ajali hiyo, Majeruhi walitolewa na kukimbizwa zahanati kwa ajili ya kupatiwa huduma ya kwanza.  Ndege iliwachukua na  kuwapeleka Dar es Salaam kwa ajili ya matibabu zaidi kwenye Hospitali ya Taifa Muhimbili.

Miili ya marehemu ilitolewa kwenye ndege na ilihifadhiwa kwa muda katika zahanati iliyopo  hifadhini.

Rais Dkt. Samia Hassan Suluhu ametuma salamu za pole kwa Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Kighoma Malima na kwa familia za marehemu.

Pia Waziri wa Maliasili na Utalii, Mohamed Mchengerwa nae ametupa salamu za pole kwa familia na wafanyakazi wa TANAPA.

Post a Comment

0 Comments