Serikali imeahidi kuipatia timu ya Yanga, ndege ya kwenda na kurudi nchini Algeria kwa ajili ya mchezo wao wa fainali.
Rais ametaka ndege hiyo kubeba wachezaji, viongozi na hata mashabiki na kwamba ni jukumu la viongozi wa TFF kuitia moyo timu hiyo
Ahadi hiyo imetolewa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan leo mara baada ya Yanga kutinga hatua ya fainalo ya kombe la Shirikisho Afrika jama.
Yanga ilifanikiwa kutinga hatua hiyo baada ya kuofunga Marumo bao 2-1 na kuitoa kwa jumla ya bao 4-1.
Mbali na ahadi ya ndege, lakini pia Rais Dkt. Samia ameahidi kulipia shilingi milioni 20 kwa kila goli litakalofungwa na Yanga kweye mchezo wa fainali dhidi ya USM Alger.
Fedha hizo hazitajali idadi na aina ya magoli yaliyofungwa, hata ya penati yatalipwa muhimu timu ipate ushindi.
Ahadi hizo zimelenga kuhakikisha Yanga inalileta kombe hilo kwa mara ya kwanza nchini.
Mechi hizo za fainali zimepangwa kuchezwa Mei 28,2023 na Juni 3,2023, ambapo Yanga itaanzia nyumbani kwenye uwanja wa Mkapa, jijini Dar es Salaam.
0 Comments