Msemaji wa Timu ya Wydad Athletic Club Mahmoud Sheriff amesema wamefurahia kupangwa na Simba.
Aliyasema hayo baada ya kuhojiwa na mwandishi wa habari kutoka kituo cha habari za michezo cha TEMARA SPORTS TV kuhusu kupangiwa Simba Sc kutoka Afrika Mashariki.
"Sisi kama Wyadad Athletic Club malengo yetu ni kutetea taji letu hili, kuhakikisha kwamba tunalibakisha Morocco nikutoe hofu tu kwamba hatuiogopi Simba Sc hata kidogo bali tunaiheshimu kama timu kubwa Africa
"Tunawajua vyema Simba Sc ni timu nzuri hasa linapokuja suala la kutumia vyema uwanja wao wa nyumbani, hakika nikiri tu wapo vizuri kwenye dimba lao la nyumbani
"Licha ya hayo lakini niwakumbushe tu kuwa sisi ndo watawala wa Soka hili la Afrika kwasasa, Simba Sc uwezo wa kumpiga nje ndani tunao, uwezo wa kumaliza mchezo wakiwa kwao tunao, hivyo niwatoe hofu tu mashabiki wa Waydad nusu fainali ni suala la muda tu kwetu.
"Baada ya kuona tumepangiwa na Simba Sc kwenye droo ile wachezaji wetu wote nimeona wakifurahi na kutabasamu, bashasha lilijaa kwenye nyuso zao, hii unafikiri ni kwasababu ya nini? hii ni kwasababu tulikua tunamtaka sana Simba Sc na malengo yetu yametimia.
"Mpaka sasa tunawafuatilia kwa ukaribu sana Simba Sc tupo nyuma yao kwa kila hatua wafanyayo, mechi yao ya jana tumeoiona, ni timu nzuri na wacheza soka safi ila tu niseme watatusamehe tukiwa na jambo letu
"Nimepata wasaa wa kuongea na Akroum binzou (Mshambuliaji hatari wa wydad) yeye alichonijibu ni kwamba wanaenda kuumaliza mchezo Tanzania kabla ya kurudi Morocco.
"Sisi ni Wydad Athletic Club, tunakuja Tanzania Kupambana."
0 Comments