Ticker

7/recent/ticker-posts

AZIZ K AONESHA THAMANI YAKE

Mchezaji ghali wa Yanga, Aziz Ki, ameonesha thamani yake baada ya kupachika goli tatu kwenye mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Kagera Sugar uliochezwa Chamazi Complex, jijini Dar es Salaam.

Mabao ya Aziz Ki Pamoja na la Fiston Mayele na Bernard Morrison yameifanya Yanga kuondoka uwanjani na alama tatu muhimu na goli tano hatua inayozidi kuwahikishia ubingwa wa pili mfululizo.


Yanga Sc ilianza kupata bao kupitia kwa Aziz Ki kwa mkwaju wa penati baada ya Fiston Kalala Mayele kuchezewa rafu ndani ya 18.

Aziz Ki aliendelea kuonyesha uwezo wake mbele ya mabeki wa upinzani kwa kupachika bao la pili kwa shuti kali la mbali ambalo lilimshinda kipa wa Kagera Sugar.

Kabla mchezo haujaishi alipachika bao lake la tatu lililomfanya aondoke uwanjani na mpira.

Fiston Mayele hakubaki nyuma katika kupachika mabao ambapo yeye alifinga bao la tatu la mchezo huo.

Hadi sasa  Mayele ndie kinara wa kupachika mabao, ambapo ana mabao 16 kwenye ligi hiyo msimu huu.

Benard Morrison aliingia kipindi cha pili na kuweza kuisaidia timu yake kupata bao la nne, alipiga  shuti kali ambalo lilizama moja kwa moja wavuni na baadae bao la tano la mchezo lilifungwa na Azizi Ki kwa mkwaju wa penati ikiwa ni bao lake la tatu.

Post a Comment

0 Comments