Ticker

7/recent/ticker-posts

BILI YA KODI YA ARDHI SASA KUTUMWA KWA SIMU


Waziri wa Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt. Angeline Mabula

Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt. Angeline Mabula amesema wamiliki wa ardhi nchini wataanza kupokea bili za kodi ya pango la ardhi kupitia simu ya mkononi

Dkt. Angelina Mabula ameyasema hayo leo Aprili 11 2023, wakati wa ziara yabmuda mfupi ya Makamu wa Rais Dkt philip Isdori Mpango ambae alisimama kwa muda katika eneo la Hungumalwa wilayani Misungwi, mkoani Mwanza ili kuzungumza na wananchi wa eneo hilo.

Makamu wa Rais yuko kwenye ziara ya siku tatu mkoani hapa.

“Ninapozungumza sasa mikoa 10 tayari imeunganishwa katika mfumo na tutaanza kupata bili zetu kupitia simu ya mkononi hivi karibuni maana watu walikuwa wakihoji kama maji waliweza kwanini ardhi wasiweze”. Alisema Waziri Mabula.

Kwa mujibu wa Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, kwa sasa kuna wataalamu  26 wanaboresha mifumo ndani ya wizara hiyo lengo likiwa kuhakikisha mifumo ya wizara inaimarika katika masuala ya malipo ili kuwawezesha wamiliki wa ardhi kuondokana na changamoto za ulipaji kodi ya pango la ardhi.

"Napenda niwahakikishie wanannchi wa Hungumalwa, Kwimba na wana Mwanza kwa ujumla kuwa zile kelele za ardhi zinaenda kuisha kwa sababu mama Samia ameiwezesha wizara” alisema Dkt Mabula.

Aidha, amesema Rais Dkt Samia Suluhu Hassan amefungua nchi na kkwamba tunahitaji  zaidi wawekezaji na kubainisha kuwa wawekezaji lazima wakute ardhi zipo na zimepangwa na kuandaliwa kwa uwekezaji.

"Niwaombe katika kutenga maeneo ya uwekezaji lazima tuhakikishe yametambuliwa na yanamilikiwa lengo ni muwekezaji akija asianze kuvutana na wananchi, halmashauri na serikali ya kijiji husika  iwe imefanya utaratibu wa kulitambua eneo na kumiliki” alisema Dkt Mabula.

Post a Comment

0 Comments