Chama cha Soka wilaya ya Songwe (SODIFA) kinasikitika kutangaza kifo cha mchezaji wa timu ya Saza fc aliyefariki baada ya kugongana na mwenzake katika kuwania mpira.
Mchezaji huyo ambae anajulikana kama Mido alikutana na kadhia hiyo kwenye mchezo wa kirafiki uliowagusisha mashabiki wa Yanga na Simba.
Lengo la mchezo huo ulikuwa ni kusheherekea sikukuu ya Pasaka.
Alifariki njiani wakati anakimbizwa hospital. Taratibu za kusafirisha mwili wa marehemu kuelekea Geita zinafanyika.
Poleni sana familia ya mpira wa miguu kwa kumpoteza kiungo fundi mkabaji. Bwana ametoa na bwana ametwaa jina lake lihimidiwe.
Taarifa hii ni kwa mujibu wa katibu Sodifa wilaya.
0 Comments