Ticker

7/recent/ticker-posts

MCHENGERWA AZINDUA BODI YA 12 YA TAFORI

Waziri wa Maliasili na Utalii,  Mohamed Mchengerwa

Bodi ya 12 ya Taasisi ya Utafiti wa Misitu (TAFORI) imezinduliwa leo mjini Morogoro na Waziri wa Maliasili na Utalii, Mohamed Mchengerwa.

Akizindua bodi hiyo waziri Mchengerwa amewataka watendaji hao waje na mkakati wa kuelimisha umma kuhusu uhifadhi wa misitu.

"Nataka niwaone mkieleza tafiti mlizofanya ili watanzania wajue wafanye nini na wachukue tahadhari gani katika uhifadhi wa misitu,” alisema Mhe Mchengerwa.


Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Dkt. Hassan Abbasi, ameeleza kuwa sekta hiyo ina mchango mkubwa kiuchumi kwani inachangia asilimia 3.3 katika Pato la Taifa huku mapato ya sekta ya misitu na nyuki mwaka jana ikiingiza zaidi ya mapato ya mauzo ya nje yanayofikia takribani Shilingi Bilioni 250.

Post a Comment

0 Comments