SERIKALI kupitia Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA) chini ya Wizara ya Maliasili na Utalii imeleta Simba wawili majike wanaoitwa Lucy na Liana katika bustani ya wanyamapori ya Ruhila iliyopo Manispaa ya Songea mkoani Ruvuma ili kuchochea utalii wa ndani
Akizungumza kwenye hafla ya upokeaji wa Simba hao iliyofanyika ndani ya bustani ya Ruhila mjini Songea, Mkuu wa Utalii kutoka Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA) Kanda ya Kusini Mashariki Kamishina Msaidizi Said Mshana amesema Simba hao wametoka hifadhi ya wanyamapori ya Sevo jijini Arusha.
0 Comments