Ticker

7/recent/ticker-posts

MZAZI AMFANYIA UKATILI MTOTO WA MWAKA MMOJA

Kamanda wa Polisi mkoa wa Iringa ACP Allan Bukumbi amewaambia   waandishi wa Habari wa Iringa juu ya matukio mbalimbali yaliyojitokeza mkoani humo kubwa likiwa la Baba kumlawiti mwanae mwenye umri wa Mwaka mmoja.

Jeshi hilo linamshikilia Amani Martin  mkazi wa kata ya Nzihi Halmashauri ya Wilaya ya Iringa  kwa tuhuma za kumlawiti mtoto wake wa kumzaa na  kumsababishia maunivu makali.

Kamanda  Bukumbi amesema  mbinu aliyotumia mtuhumiwa ni kumshika mtoto kwa nguvu  na kumfanyia kitendo hicho wakati wakiwa shambani baada ya mama wa mtoto kuondoka kwenda kuokota kuni na kumuacha mtoto akiwa na baba yake.

Amesema kiini cha tukio hilo bado kinachunguzwa na mtuhumiwa amekamatwa na taratibu za kisheria zinaendelea kuchukuliwa dhidi yake.

Pia Jeshi la Polisi mkoani Iringa linawashikilia watuhumiwa  watatu kwa makosa ya kumiliki silaha kinyume na utaratibu katika maeneo tofauti ya mkoa huo huku baadhi yao wakikodisha silaha hizo  kwa watu kinyume na sheria.

Post a Comment

0 Comments