Ticker

7/recent/ticker-posts

BALOZI POLE POLE AHAMISHIWA CUBA

Balozi Humphrey Polepole

Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, amefanya mabadiliko ya vituo vya kazi kwa mabalozi wawili pamoja na kuteua balozi mpya mmoja.

Amempangia Balozi Humphrey Herson Polepole kuiwakilisha Tanzaniia nchini Cuba.

Kabla ya uteuzi huo Polepole, alikuwa Balozi wa Tanzania nchini Malawi.


Aidha Rais Dkt. Samia amemteua Jeneral mstaafu, Yacoub Mohamed kuiwakilisha Tanzania katika Falme za Kiarabu (UAE), kabla ya uteuzi huo Balozi Mohamed aliwa balozi wa Tanzania nchini Uturuki.

Pia amemteua Bw. Iddi Seif kuwa Balozi na moja kwa moja amempangia kuiwakilisha Tanzania nchini Uturuki, kabla ya uteuzi huo Balozi Bakari alikwa Konseli mkuu Dubai.

Mabalozi hawa wataapishwa mara baada ya tarehe ya hafla hiyo kutangazwa.

Post a Comment

0 Comments