Ticker

7/recent/ticker-posts

VIJANA WAPEWA FURSA KWENYE KILIMO

 


Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwakabidhi Vijana mfano wa hundi ya Sh. Milioni 200 , Chinangali Mkoani Dodoma

SERIKALI ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan imeendelea kuwatazama vijana kwa jicho la upendo baada ya kuamua kuwaachia jukumu la kuendesha kilimo cha mashamba makubwa ya pamoja (Block Farming).

Jana Rais  Dkt. Samia alizindua Programu ya Kilimo cha Mashamba makubwa ya pamoja Chinangali Mkoani Dodoma, ambapo pamoja na mambo mengine aliwakabidhi vijana hao mfano wa hundi ya shilingi milioni 200 maalum kwa ajili ya shughuli za kilimo kwa vijana.

Sehemu ya mashamba makubwa 
Dhamira ya serikali ni kuhakikisha kilimo kinachangia fedha nyingi kwenye pato la taifa, lakini pia kinaondoa changamoto ya ajira kwa vijana. Mradi huo utadumu kwa miaka nane kutoka 2022-2030.

Post a Comment

0 Comments