Pamoja na mambo mengine, Sheikh Kipozeo aliwataka waislamu kutojiweka karibu na wanaume laini laini (Mashoga) labda kama wanataka kuwapa neno la Mungu.
Aliyasema hayo katika kongomano la kuukaribisha mwezi Mtukufu wa Ramadhani na mmomonyoko wa maadili.
“Nilishawahi kuwavua cheni na hereni wanaume na nikawaambia wasirudie tena, wewe kama mwanaume unavaa chezi au hereni ya nini, halafu bila haya unaingia nayo msikitini.
“Hawa hawa wanaume laini laini utawakuta eti na wao wamefunga na wanajilegeza kabisa kuwa ‘tumefungaaa’, tukae nao mbali labda kama tunataka kuwapa neno la Mungu.”
Mvaa hereni |
“Ramadhani kwetu iwe chou cha maisha, tutakavyoishi ndani ya mwezi mtukufu wa Ramadhani ndio tuishi pia kwenye siku nyengine, kule Zanzibar kuna mama mmoja ameoa wanawake wenzake wanne nah apo Magomeni kuna mwanaume anataka kuolewa, sasa wanawake wataolewa na nani, ni mambo ya aibu.”
0 Comments