Nembo ya Simba Sc
WAWAKILISHI wa Tanzania kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika, Simba SC leo inacheza mechi ya jasho na damu dhidi ya Horoya Athletic Club ya Guinnea.
Mchezo huu si wa kawaida kutokana na umuhimu wake, Simba inahitaji pointi tatu tui li ijihakikishie kwenda hatua yar obo fainali.
Kwa upande wake Horoya pia inazihitaji pointi hizo ili iingize mguu mmoja ndani yah atua yar obo fainali, kwa lugha nyepesi unaweza kusema ni mchezo wa kisasi ambao unaweza usitawaliwe na udambwi udambwi zaidi ya kila upande kusaka matokeo.
Sare haitakuwa na maana kwa Simba, zaidi itakuwa imejitengenezea mazingira magumu kwani itatakiwa kuifunga Raja Casablanca kwao, kitu ambacho ni kigumu.
Pamoja na mambo mengine Simba ndio inapewa nafasi kubwa kwenye mchezo huu kutokana na matokeo yake ya hivi karibuni, hata hivyo Horoya Athletic Club, pia ikijulikana kama Horoya Conakry au H.A.C., yenye makazi yake mjini Conakry, Guinea ikicheza katika Ligue 1 Pro, daraja la juu katika mfumo wa ligi ya soka ya Guinea.
ilianzishwa mnamo 1975 si timu rahisi.
Timu hii ambayo katika mchezo wa awali uliofanyika kwenye uwanja wake wa 28 Septembre, uliopo katika mji wa Conakry, iliifunga Simba bao moja.
Baadhi ya wachezaji wa Simba |
HISTORIA YA HOROYA AC
Afrinews Swahili imeiona haja ya kukupa historia ya timu ya Horoya AC na baada ya mchezo huo tutakuletea historia kamili ya klabu ya Simba.
Rais wa Klabu hii anaitwa Antonio Souaré
Manager wa Timu hii ni Lamine N’diane
Moja ya Historia yao kubwa kwenye michuano hii ni Mnamo 2014, pale walipowaondoa washindi wa pili wa Kombe la Dunia la Klabu ya FIFA ya 2013 Raja Casablanca katika raundi ya pili ya kufuzu kwa Ligi ya Mabingwa ya CAF ya 2014.
Mwaka 2018, baada ya kushika nafasi ya pili katika hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika, klabu hiyo ilitinga robo fainali kwa mara ya kwanza katika historia yake, ambapo ilipoteza dhidi ya Al Ahly SC kwa jumla ya mabao 4-0 (0-0 mjini Conakry na 4-0 huko Cairo).
Jina Horoya maana yake ni-Uhuru katika lugha za kienyeji za Guinea na Kiarabu. Neno hili linatokana na ushawishi mkubwa na umuhimu wa waarabu kwa jamii ya Guinea.
Wanatumia jezi zenye rangi nyekundu na nyeupe. kama tu ilivyo kwa Simba Sports Club Wekundu wa Msimbazi
Kwa Horoya rangi hii Nyekundu,ni ishara ya damu ya mashahidi kwa mapambano ya uhuru, na nyeupe ikiwa na maana ya usafi mkubwa na matumaini.
Tukitazama Historia yao kwenye Mashindano mbalimbali Klabu hii Kitaifa kwenye upande wa Ligi ya Horoya iitwayo Ligi one Pro wamekuwa mabingwa mara 20, nayo ni miaka ya 1986, 1988, 1989, 1990, 1991, 1992, 1994, 2000, 2001, 2011, 2012, 2013, 2014, 2016, 2017, 2018, 2019, 2020, 2021, 2022
Mabingwa wa Guinée Coupe Nationale mara 9
wakiwa mabingwa wa Guinean Super Cup mara 6
nayo ni miaka ya 2012, 2013, 2016, 2017, 2018, 2022
kwenye nchi ya Guinnea mahasimu wao wakubwa ni Santoba Fc-na hizi ndizo Timu kubwa ndani ya Guinnea zikiwa na mafanikio makubwa-na wanapokutana mechi yao huitwa Conakry Dabi.
Kiwango chao kwenye Michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika tukiwatazama.
Baadhi ya wachezaji wa Horoya
Mwaka 2000 – waliishia Raundi ya kwanza
2002 – wakaishia hatua za awali
2012 – wakaishia hatua ya kwanza
2013 – wakaishia Hatua ya kwanza
2014 – wakaishia hatua za mtoano
2016 – wakaishia hatua ya kwanza
2017 – wakaishia hatua ya kwanza –
2018–19 wakaishia Robo Fainali, mwaka ambao Simba pia waliishia katika Hatua hizo
2019–20 – wakaishia Raundi ya kwanza wakati mwaka huo Simba wakiishia Hatua za awali
2020–21 – wakaishia hatua ya makundi, mwaka ambao Simba aliishia Robo Fainali
2021–22 – wakaishia hatua za makundi, mwaka ambao Simba waliishia Hatua ya Pili
Kwenye Ligi kuu ya nchini Guinnea Ligue 1 Pro ambayo inashindaniwa na Vilabu 14 pekee, mpaka sasa wamecheza michezo 13 wakiwa kileleni mwa msimamo kwa kukusanya alama 29 ambapo katika michezo hiyo wameshinda 9 wamepoteza miwili na kudroo miwili-katika michezo mitano ya mwisho waliyocheza mpaka sasa wameshinda yote.Kikosi cha Horoya AC
Kundi lao linajumuisha Timu za Raja Casablanca ya Morocco, Vipers United ya Uganda, Simba Sc ya Tanzania, na wenyewe Horoya Ac.
0 Comments