Ticker

7/recent/ticker-posts

RAIS SAMIA ATAKA TANZANIA KUWA GHALA LA CHAKULA AFRIKA

  



Rais Dkt. Samia akizindua AGRF
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan, amezindua Jukwaa la Mfuko wa Kilimo Afrika (AGRF), huku akisisitiza kuwa dhamira yake ni kuona Tanzania inakuwa ghala la chakula Barani Afrika ifikapo 2030.

Uzinduzi huo wa Jukwaa la Mfuko wa Kilimo Afrika ni maandalizi ya mkutano mkubwa wa kilimo Afrika na duniani ambao unatarajiwa kufanyika Tanzania, Septemba mwaka huu. 

Katika uzinduzi huo, Rais Dkt. Samia amesema matarajio yake ni kuona sekta ya kilimo inachangia pato la taifa kwa asilimia 30 hadi ifikapo mwaka 203, jambo ambalo amesema linawezekana.


Viongozi mbalimbali walioshiriki kwenye uzinduzi huo

Rais Samia ameyasema hayo , Ikulu jijini Dar es Salaam wakati akizindua Jukwaa hilo, pamoja na kuutangaza rasmi  mkutano huo uliopangwa kufanyika Septemba 5-8 nchini.

Katika uzinduzi huo umesema Tanzania ina fursa ya ardhi yenye rutuba na vyanzo vya maji hivyo vikitumika ipasavyo, ni wazi sekta ya kilimo itachochea pato la taifa kukua kwa kasi.

Amesema kilimo kinachangia uchumi wa Tanzania kwa asilimia 25 ambacho ni muhimu katika kukuza maendeleo, hivyo jitihada zake ni kuona mchango huo unaongezeka kwa kasi kubwa.


Rais Dkt. Samia akizungumza kwenye uzinduzi huo


 

Post a Comment

0 Comments