Mshambuliaji hatari wa Yanga, Mayele |
Hakuna ubishi kikosi cha Yanga kwa sasa kimekamilika kila idara, kila mchezaji anaepata nafasi ni hatari anapokuwa na mpira.
Uhatari wa kikosi ch Yanga unasukumwa zaidi na ari na kiu ya mafanikio waliyo nayo wachezaji na benchi la ufundi, hakuna anayetaka kuharibu.
Pamoja na ukweli huo, lakini ipo dhana pia Yanga ya sasa imeweka uwezo wake wote kwenye jezi yake ya rangi nyeusi, hii ni dhana ambayo kamwe haiwezi kuoewa nafasi kubwa ingawa hakuna linaloshindikana.
Timu hii yenye maskani yake Jangwani kesho inaingia uwanjani kusaka alama tatu ambazo zitaivusha na kuipeleka kwenye hatua yar obo fainali.
Yanga inakutana na timu ya monastery kutoka Tunisia, wapinzani hawa wa Yanga yenyewe tayari imejihakikishia kusonga mbele kutokana na matokeo mazuri iliyoyapata kwenye michezo yake yote ikiwa ni pamoja na ule waliocheza na Yanga mwezi uliopita.
Kwenye mchezo huo Yanga ambayo iko kundi D, ilipoteza mchezo wake huo ambao ndio ulikuwa wa kwanza wa kombe la shirikisho kwa hatua ya makundi kwa kufungwa bao 2-0.
Yanga sc ilingia kwenye mchezo huo na mpango kazi wa kucheza mpira huku ikiamini itapata ushindi na kuwa na umiliki mkubwa wa mpira lakini kukosekana kwa umakini katika kuokoa mipira iliyokufa hasa kona na faulo ilisababisha Monastri kupata mabao mawili mapema zaidi dakika za 10 na 16 kupitia kwa Mohamed saghraoui na Boubacar Traore yote yakifungwa kwa kichwa.
Kikosi cha Yanga kina alama saba kikiwa nyuma ya Monastry na kwenye mchezo wake wa kesho klabu hiyo ya Jangwani itahitaji ushindi ili kujihakikishia hatua ya kwenda robo fainali.
Kila la heri Yanga.
0 Comments