MSEMAJI COASTAL UNION ATOA NENO FACE BOOK
Katika ukurasa wake wa Facebook, Msemaji na shabiki wa Coastal Union ya Tanga, Jonathan Tito ameandika, hongera sana shabiki mwenzangu wa Coastal Union FC.
Najua kuna ambao hawawezi kuzungumzia mazuri yako na kukupamba kwasababu unatoka Tanga ila kwa ushamba wao ungetokea labda Dar hata kukuabudu wangekuabudu.
Ila umefanya makubwa sana!
Mfano;
(1) Ligi Kuu Tanzania Bara ni namba tano Africa na duniani namba 39.
(2) Mwaka 2019 tumecheza AFCON kwa mara ya pili baada ya miaka 39.
(3) Vituo vya soka Mnyanjani na Kivukoni.
(4) Udhamini wa Azam TV na mengine mengi.
Pamoja na hayo yote hakuna gazeti lililowahi kuandika mazuri yake ila katafute mabaya sasa, mpaka makosa ya waamuzi analaumiwa yeye!
0 Comments