Ticker

7/recent/ticker-posts

"NILIVUMILIA MATESO YA NDOA KWA KUIGOPA JAMII"

Coletha Raymond

Nilichelewa kuondoka katika ndoa iliyojaa matukio yasiyovumilika kwa fikra kuwa jamii na wazazi watanionaje nikiachana na ndoa lakini maji yaliponifika shingoni nilikimbia

Mwigizaji maarufu Tanzania, Coletha Raymond ameeleza namna alivyoondoka kwenye ndoa yake baada ya kuzidiwa na matukio yasiyovumilika kutoka kwa mumewe

Coletha amesema haikuwa rahisi kuachana na  ndoa yake kwani alikuwa anampenda sana mumewe, alijaribu kuvumilia lakini baadae aliona ipo haja ya kuendelea na maisha yake mwenyewe baada ya kuona hakukuwa na mabadiliko ya mumewe kujirekebisha

Coletha ameingia ndani kwa kusema miongoni mwa kitu kilichokuwa kinamchelewesha kuondoka kwenye ndoa yake licha ya kupigwa matukio ya mara kwa mara ni fikra za kwamba jamii itanionaje, wazazi watanichukuliaje nikiondoka kwenye maisha ya ndoa, lakini baadae alijikuta anapata nguvu na kumuacha mumewe ambaye amezaa naye mtoto mmoja wa kike

"Kuhusu kuolewa tena mimi ni mwanamke na ndoa hatuolewi kwa fasheni lakini inaleta stara kwa mwanamke unayejiheshimu, kama ikitokea naweza nikaolewa tena lakini siyo lazima sana kwangu yani siyo kitu ambacho nimeweka akilini, mawazo, kila kitu kwamba ndoa! ndoa! ndoa! hapana, kwangu ije tu ikija fresh isipokuja fresh maisha yataendelea"

"Sipendi mwanaume ambaye nimemzidi umri ingawa sikatazi kwa wanaofanya wafanye kwa manufaa yao na siyo mbaya kwanza kila mtu na mapenzi yake

Sifa kubwa ya mwanaume ninayemtaka kwanza awe mchapakazi, sitaki wale wanaume magoigoi tu, namtaka mwanaume mwenye hofu ya Mungu, nataka mwanaume mwenye upendo wa kweli kwangu, mwanaume atakayenithamini mimi kama mwanamke kwake na atakayenipa nafasi ya kunisikiliza na mwenye heshima"- amesema Coletha Raymond.

Post a Comment

0 Comments