Ticker

7/recent/ticker-posts

MCHECHU AKABIDHIWA JUKUMU ZITO ZAIDI

  

Nehemia Mchechu


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan amefanya uteuzi kama ifuatavyo:-

 

1.         Amemteua Bw. Nehemia Kyando Mchechu, kuwa Msajili wa Hazina.  Kabla ya uteuzi huo Bw. Mchechu alikuwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC).  Bw. Mchechu anachukua nafasi ya Bw. Mgonya Benedicto ambaye atapangiwa kazi nyingine.  

 

2.         Amemteua Bw. Hamad Abdallah, kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC). Kabla ya uteuzi huo, Bw. Abdallah alikuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Gimcoafrica Limited na anachukua nafasi ya Bw. Mchechu ambaye ameteuliwa kuwa Msajili wa Hazina.

 

3.         Amemteua Bw. Mussa Mohammed Makame, kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC).  Kabla ya uteuzi huo, Bw. Makame alikuwa Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC), na pia ni Mshauri Mwelekezi wa masuala ya mafuta na gesi nchini Tanzania. Bw Makame anachukua nafasi ya Dkt. James Mataragio ambaye atapangiwa kazi nyingine.

  

Uteuzi huu ni kuanzia tarehe 24 Februari, 2023.

 

Taarifa hii imetolewa na Zuhura Yunus

Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu

Post a Comment

0 Comments