| Mwenyekiti wa JET, Dkt. Ellen Otaru |
NA MWANDISHI WETU
Viongozi wa juu wa Chama cha Waandishi wa Habari za Mazingira Tanzania (JET), wameipaisha Tanzania kimataifa kwa kuteuliwa kuongoza taasisi za mazingira duniani.
Mwenyekiti wa chama hicho, Dkt. Ellen Otaru-Okoedion, ameteuliwa kuwa mwakilishi wa mashirika yasiyo ya Kiserikali Barani Afrika kwa sasa hadi sasa baada ya Mkutano wa COP17.
Akizungumzia nafasi hiyo Dkt. Ellen amesema kazi yake ni kuhakikisha anaipigania nchi yake ya Tanzania kimataifa kwenye eneo la mazingira.
“Jukumu langu ni moja tu, ni kuhakikisha naipambania Tanzania kimataifa na nashukuru kwa kupata nafasi hiii na. Tupo pamoja kuitangaza Tanzania,”amaesema.
Aidha dunia imemuona Mkurugenzi wa JET, John Chikomo, ambae ameteuliwa kuwa Mratibu wa Kitaifa kwa upande wa Mashirika yasiyo ya Kiserikali (NGO National Coordinator) wa UNCCD kwa Tanzania, nafasi itakayoiwezesha nchi kusimamia kwa karibu utekelezaji wa mikataba na ajenda zinazolenga kukabiliana na changamoto za mmomonyoko wa ardhi na ukame.
| Mkurugenzi wa JET, John Chikomo |
Mkataba huo ni kati ya Mikataba mitatu iliyopitishwa kwenye mkutano wa Mazingira na Maendeleo (The United Nations Conference on Environment and Development-UNCED uliofanyika nchini Brazil mwaka 1992 na kwamba Tanzania ikiwa ni mwanachama imekuwa ikitekeleza majukumu yake kupitia mipango kazi ya muda mfupi, wa kati na mrefu, ikilenga kupunguza kasi ya mmomonyoko wa ardhi na athari za ukame.
“Tanzania imeendelea kutekeleza majukumu yake kama nchi mwanachama wa Mkataba katika Nyanja mbalimbali. Katika kutekeleza majukumu chini ya Mkataba, mwongozo na makubaliano ya nchi wanachama (COP Decisions), nchi wanachama zinapaswa kuandaa mpango kazi wa utekelezaji na hili linasisitizwa katika kifungu cha 9 (1) cha Mkataba (Article of the Convention.
“Lengo la Mpango kazi huu ni kuainisha visababishi vya kuenea kwa hali ya jangwa na kubuni njia muafaka za kupambana na visabishi hivyo na madhara yake hususan ukame. Tanzania iliandaa Mpango kazi wa Kitaifa wa Kupambana na Kuenea kwa Hali ya Jangwa na Ukame na kufanyiwa mapitio,”.
Amesema utekelezaji wa Mpango Kazi huo umegawanyika katika sehemu tatu ambazo ni muda mfupi, muda awa kati na muda mrefu (1-2/3-5 na >5) huku majukumu ya utekelezaji yakiwa yametolewa katika ngazi zote za kiutendaji (Wizara za Kisekta, Mashirika ya Kiserikali, Washirika wa Maendeleo, Asasi zisizo kuwa za Serikali na Sekta Binafsi.
0 Comments