Na JIMMY KIANGO
Kutosimamiwa kikamilifu kwa Sheria ya Misitu yam waka 2002 iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2022 sanjari na sheria ya Usimamizi wa Mazingira yam waka 2004 iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2025 pamoja na kanuni zake, kumechangia kupotea kwa zaidi ya hekta 460,000 za misitu kila mwaka nchini Tanzania.
Kwa mujibu wa ripoti kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira, hali hiyo husababishwa na uvunaji wa miti usiozingatia sheria pamoja na ukataji wa miti kwa aji ya matumizi ya kuni na mkaa.
Kuteketea kwa kiasi hicho cha hekta za misitu husababisha athari mbalimbali ikiwemo kukauka kwa vyanzo vingi vya maji, ukame na mabadiliko ya tabia nchi kwa ujumla.
Changamoto hii inapaswa kutatuliwa kwa haraka ili kuepusha hatari zaidi kwa ustawi wa uhai wa mazingira na wananchi na hasa ikizingatiwa kuwa hali si nzuri kwa nchi nyingi za Afrika, ambapo inaelezwa kuwa kuanzia mwaka 2010 hadi 2020 hekta milioni 3.9 zilipotea barani Afrika huku Tanzania ikichangia asilimia 12.
Mkuu wa Idara ya Mawasiliano wa Shirika la Uhifadhi wa Mazingira Duniani (WWF), ofisi ya Tanzania, Joan Itanisa, anasema takwimu za mwaka 2019 zinaonesha Tanzania inapoteza mikoko 479
Kila mwaka, sawa na asilimia sita, huku nusu ya vyanzo vya maji vikiendelea
Kukauka.
Joan aliongeza kuwa mmomonyoko wa udongo umefikia asilimia 61 ya
ardhi nchini na kwamba kupitia mkakati wa urejeshaji wa uoto wa asili na kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi duniani ifikapo mwaka 2030 (WWF 2030).
Joan amesema kiasi cha dola za Marekani trilioni 13 zinatarajiwa kuwekezwa kwenye mpango huo wa
urejeshaji wa uoto wa asili na kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi duniani.
Amesema iwapo fedha hizo zitapatikana, inakadiriwa kuwa kiasi cha hekta bilioni 18 za miti zitarejeshwa na kiasi cha watu bilioni 4.5 duniani kote watanufaika na uamuzi huo wenye lengo la kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi na kuhakikisha mazingira asili yanabaki salama kwa kizazi cha sasa na kizazi kijacho.
Mkuu wa Idara ya Mawasiliano wa Shirika la Uhifadhi wa Mazingira Duniani (WWF), ofisi ya Tanzania, Joan Itanisa
Joan alisema katika mpango huo wa 2030, nchi 193 zinatarajiwa
kushiriki kwa kuandaa sera na utekelezaji na wanatarajia hadi kufikia mwaka 2030, mifumo ya chakula na kilimo
itakuwa imeimarika na kuwezesha asilimia 800 ya uzalishaji wa chakula kuwa na matokeo
chanya.
“Ifikapo mwaka 2030, uwezo wa kustahimili mfumo wa ikolojia, unaweza kuathiriwa na hatari ya hali ya hewa na kupunguza uzalishaji kutokana na
hewa ukaa, na suluhu ya hilo ni kurejesha asili, mabadiliko ya kisekta na matumizi ya nishati safi,” alisema.
Joan alisema mpango huo unatarajia kuweka kipaumbele kwenye kulinda
viumbe hai walio hatarini kutoweka duniani, wakiwamo simba, faru weusi,
mbwa mwitu na samaki aina ya papa potwe.
0 Comments