Ticker

7/recent/ticker-posts

VISION PLUS YAITANGAZA TANZANIA IRAQ, YAFURAHISHWA NA KAZI ZA RAIS SAMIA

Dot. Datoo akitoa huduma ya utabibu wa mamcho kwa mmoja wa wananch wa Iraq

 NA MWANDISHI WETU

 

Taasisi binafsi ya Vision Plus inayotoa huduma ya afya ya macho na miwani, imefanikiwa kuitangaza Kimataifa kutokana na kutoa huduma za kibingwa za macho nchini Iraq.

 

Hatua hiyo imewagusa wananchi wa nchi hiyo waliopatiwa huduma hiyo na taasisi hiyo ya Vision plus. 

 

Akizungumza na mtandao huu, Mtendaji Mkuu wa Vision Plus, Dkt. Hassanal Datoo alisena kuwa nafurahia kuitangaza kimataifa pamoja na kuwaeleza Wananchi wa Iraq kazi kubwa iliyofanywa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.

 

Dkt. Datoo anasema ametekeleza dhamira yake hiyo pale alipopata nafasi ya kuhojiwa na maafisa wa ofisi ya Wqfu wa Kishia wenye makazi yake nchini Iraq (

ATABAT)

 

Dkt. Datoo wa pili kutoka kushoto akiwa pamoja na vada wa afya ya macho nchini Iraq.

"Nilipata heshima ya kuhojiwa na maafisa kutoka ATABAT (Ofisi ya Waqfu wa Kishia – Iraq) hii ni  Taasisi inayosimamia maeneo Matakatifu ya Kishia na kuratibu shughuli za mashirika yasiyo ya kiserikali (NGO's) wakati wa Arbaeen ya Imam Hussain.

 

"Pamoja na mambo mengine, lakinj mazungumzo yetu yalijikita katika mchango wangu kwa wa muda mrefu wa kuziwekea kambi za macho Zanzibar ambazo kwa miaka mingi nimekuwa nikitoa huduma za bure za matibabu ya macho kwa mahujaji na jamii za wenyeji wakati wa tukio hili takatifu.

 

"Ilikuwa ni heshima kubwa kuwasilisha maono yangu  ya huduma na kuchunguza manufaa mapana ya mpango huu.

 

"Lakini pia kwa umuhimu mkubwa niliwapa historia fupi ya Zanzibar na maendeleo ya kasi yanayopatikana Tanzania na namna Rais Dkt.  Samia anavyoleta maendeleo kwa kasi."

 

Post a Comment

0 Comments