NA MWANDISHI WETU-MOROGORO
Mkurugenzi wa Tume ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi (PDPC), Dkt. Emmanuel Mkilia amesema kila mtu, taasisi ama Ofisi ya Umma ama binafsi inayojihusisha na ukusanyaji na uchakataji wa taarifa, inapaswa kujisajili kwenye tume hiyo.
Amesema, kwa mujibu wa kifungu cha 14 cha Sheria ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi nchini, kutojisajili ni kosa.
Dkt. Mkilia ametoa kauli hiyo kwenye kikao cha PDPC na Wahariri wa vyombo vya habari Machi 1,2025, mkoani Morogoro.
Amesema, PDPC iliyozinduliwa Aprili 3, 2024, kwa lengo la kumlinda mwenye taarifa, kusimamia sheria ya ulinzi na kufanya uchunguzi wa ukiukwaji wa haki za faragha.
0 Comments