Ticker

7/recent/ticker-posts

KAZI INAENDELEA KWA VITENDO UBUNGO, WANAFUNZI WOTE WARIPOTI SHULENI,DC BOMBOKO AFURAHISHWA NA HATUA HIYO

 

Mkuu wa wilaya Ubungo, Hassan Bomboko akizungumza wakati  wa ziara yake wilayani humo.

#KAZIINAONGEA

Mkuu wa wilaya Ubungo Hassan Bomboko ameendelea kuiishi kwa vitebdo kauli mbiu ya Rais Dkt. Saamia Suluhu Hassan ya 'KAZI IENDELEE' ambapo leo Januari 13,2025 akiwa na kamati yake ya Ulinzi na Usalama ya  Wilaya hiyo  ametembelea na kukagua shule zilizopo katika wilaya yake.

 

 Lengo la ziara hiyo pamoja na mambo mengine ni kujionea namna shule zote wilayani humo zilivyo anza kupokea wanafunzi wa Awali, darasa la kwanza na kidato cha kwanza kwa muhula wa masomo wa mwaka 2025

 

Katika ziara hiyo Mheshimiwa Bomboko ameeleza namna ambavyo Serikali ya Awamu ya Sita inayoongizwa na Rais Dkt. Samia ilivyo wekeza kwa kiasi kikubwa katika sekta ya elimu kwa kujenga miundombinu ya madarasa, vyoo, maabara, nyumba za walimu mabweni na miundombinu mingine na kusababisha  mazingira ya kujifunza kuwa ni mazuri na salama.

 

Aidha Bomboko amempongeza Rais kwa kuwa na dhamira njema na maono makubwa ya kuwekeza fedha zaidi ya Bilioni 29 katika sekta ya elimu ambapo katika fedha hizo shilingi Bilioni 19 ni kwa ajili ya elimu ya sekondari huku Bilioni 10 zikielekezwa kwenye elimu ya  msingi.

 




Post a Comment

0 Comments