NA MWANDISHI WETU,AFRINEWSSWAHILI -RIYADH
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Terra Global Capital la California nchini Marekani, Michael A. Cullen, D. Phil, leo Desemba 6,2024 ametembelea banda la maonesho la Chama cha Waandishi wa Habari za Mazingira Tanzania (JET) kujionea shughuli zinazofanywa na chama hicho.
Mwenyekiti wa JET, Dkt. Ellen Otaru na Mkurugenzi wa chama hicho wako Riyadh, Saudi Arabia wakishiriki mkutano wa COP 16.
Pamoja na mambo mengine Phil amekutana na viongozi wa chama hicho na kujadiliana kuhusu miradi mbali mbali inayohusu biashara ya hewa Ukaa.
Aidha viongozi hao kwa pamoja wameyaangazia kwa umakini mkubwa maeneo ya ushirikiano kati ya JET na Terra Global Capital katika mkutano wa COP16 unaoendelea nchini humo.
0 Comments