Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Dkt. Doto Biteko (kushoto) akimkabidhi Mkurugenzi Mkuu wa TPA, Plasduce Mbosa zawadi ya kikombe cha ushindi wa tuzo ya mwajiri bora wa mwaka.
NA MWANDISHI WETU
Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) imetwaa kwa mara ya tatu mfululizo Tuzo ya Mwajiri bora wa mwaka kwenye Sekta ya Umma katika halfa ya Usiku wa Tuzo kwa Mwajiri bora kwa mwaka 2024, uliofanyika mwishoni mwa wiki iliyopita, jijini Dar es Salaam.
Tuzo hizo zilitolewa na Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Dkt. Doto Biteko aliyemwakilisha Makamu wa Rais wa Dkt. Phillip Mpango.
Katika usiku huo wa Tuzo, TPA imetwaa jumla ya Tuzo Tano ambazo ni Tuzo ya mshindi wa kwanza Mwajiri bora wa mwaka kwenye Sekta ya Umma, Tuzo ya Mwajiri Bora Mzawa (Local Employer Award) mshindi wa kwanza, tuzo ya mshindi wa pili wa Jumla sekta zote (2nd Runners -up award), tuzo ya wanaofanya vizuri zaidi ( Club of best performers ), tuzo ya mwanachama wa ATE kwa muda mrefu
kwa Taasisi za Umma wa mwaka 2024 na tuzo ya Mwajiri bora wa Ndani ya Nchi.
Tuzo hizi hufanyika kila mwaka na kuandaliwa na Chama cha Waajiri Tanzania (ATE) kwa ajili ya Waajiri wa Sekta za Umma na Binafsi ambao wamefanya vizuri zaidi katika mwaka husika.
0 Comments