Ticker

7/recent/ticker-posts

JET YAIPEPERUSHA BENDERA YA TANZANIA VEMA SAUDI ARABIA

Baadhi ya wajumbe wa Tanzania katika mkutano wa 16 wa nchi wanachama wa Mkataba wa Kupambana na kuenea kwa Hali ya Jangwa na ukame unaoendelea mjini Riyadh, Saudi Arabia 
 

NA MWANDISHI WETU- RIYADH

Ujumbe wa Tanzania katika mkutano wa 16 wa nchi wanachama wa Mkataba wa Kupambana na kuenea kwa Hali ya Jangwa na ukame unaoendelea mjini Riyadh, Saudi Arabia umeliwakilisha vyema taifa.

 

Katika mkutano huo Tanzania inaongozwa na Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Khamisi Hamza Khamis.

 

Tanzania inautumia mkutano huo kuieleza Jumuia ya Kimataifa kuhusu jitihada zinazochukuliwa na Serikali na Mashirika yasiyo ya Kiserikali katika kudhibiti hali ya kuenea kwa jangwa na ukame.

 

Chama cha Waandishi wa Habari za Mazingira Tanzania (JET) ni miongoni mwa taasisi zinazoshiriki kwenye mkutano huo na kimekuwa kikiendelea kuonesha kazi mbalimbali ambazo inafanya nchini Tanzania katika kueleimsha jamii kupitia vyombo vya habari. Ushiriki wa JET umekuwa ni kiunganishi muhimu kwa nchi, kwa kuwa inapeleka taarifa kuhusu majadiliano na makubaliano ambayo yanaendelea kwenye mkutano huu.

 

Sambamba na hilo pia JET imeshiriki katika kikao kazi Pamoja na ujumbe wa Tanzania na Mtendaji Mkuu wa Mkataba wa Ramsar Dkt. Musonda Mumba. Mkutano huu wa uwili baina ya ujumbe wa Tanzania na Sekretariati ya Mkataba wa Ramsar una manufaaa makubwa kwa Tanzania katika kuhifadhi maeneo ya ardhi oevu yaliyopo manufaa ya kizazi cha sasa na cha baadae. 




Post a Comment

0 Comments