Ticker

7/recent/ticker-posts

ORXY YAUNGA MKONO JUHUDI ZA SERIKALI

 

Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni hiyo Benoit Araman akigawa jiko la pesi kwa mwananchi.

Na. MWANDISHI WETU

Kampuni ya gesi ya Orxy Gesi iekuwa mdau mkubwa kwenye kusambaza nishati safi ya kupikia nchini, ambapo imekuwa ikishirikiana na serikali katika kufanikisha mkakati wa nishati safi ya kupikia.

 

Katika kufanikisha hilo kampuni hiyo imeweza kugawa mitungi ya gesi kwa makundi mbalimbali wakiwemo wabunge na hata Wanahabari.

 

Katika kuendelea kuiunga mkono serikali kuhakikisha watanzania wote wanatumia nishati safi ya kupikia kampuni ya Oryx Gas Tanzania, imekuwa ikitoa mitungo ya gesi kutokana na kuthamini umuhimu wa nishati safi ya kupikia pamoja na kumuunga mkono Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.

 

 

Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni hiyo Benoit Araman amesema lengo la kugawa mitungi ya gesi na majiko ni mwendelezo wa kuunga mkono juhudu za serikali ambayo imedhamiria kuhakikisha wananchi wanatumia nishati safi ya kupikia.

 

Sambamba na hayo Araman amesema faida ya kutumia gesi ya Oryx kwenye taasisi mbalimbali, inasaidia kuongeza ufanisi katika uzalishaji na kupunguza muda wa taasisi husika kutafuta nishati nyingine kama kuni na mkaa, kulinda mazingira, Afya na kuwalinda Wanawake na watoto kuumia wakitafuta kuni.

 

“Oryx imekuwa na kampeni maalum ya kuhakikisha inaiwezesha jamii kutumia nishati safi ya kupikia, hivyo imekuwa ikigawa mitungi bure kwa makundi mbalimbali katika jamii.”

 

Post a Comment

0 Comments