Hati ya kusafiria ya rafa wa Marekani ambe ametajwa kuhusika na jaribio la kuipindua serikali ya Kongo-DRC |
DRC-KONGO
Marekani imekana kuwa na uhusiano na raia wake wa Marekani walionaswa katika jaribio la kutaka kumpindua Rais wa Kongo, Felix Tshisekedi. Balozi wa Marekani nchini Kongo, Lucy Tamlyn amesema nchi yake haina uhusiano wowote na watu hao kwenye harakati zao hizo za kutaka kuipindua serikali.
Jana Mei 19,2024 Jeshi la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo lilifanikiwa kuzuia jaribio la mapinduzi lililolenga kuteka Ikulu ya Taifa na makazi ya Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Uchumi Vital Kamerhe, kama ilivyoripotiwa na televisheni ya taifa ya nchi hiyo RTNC.
Hatua za haraka za wanajeshi wa Jeshi linaloitii serikali zilirejesha utulivu kwa umma ndani ya muda mfupi na kusababisha kuzuiliwa kwa waasi kufanikisha jaribio lao hilo.
Jaribio la mapinduzi linahusishwa na wafuasi wa vuguvugu la "New Zaire", linaloongozwa na Christian Malanga, ambaye inasemekana alianzisha serikali yake akiwa uhamishoni nje ya nchi.
Kulingana na mradi wa uchambuzi wa Atum Mundi, Malanga, ambaye aliishi Marekani, alidaiwa kushiriki katika jaribio hilo yeye mwenyewe akiwa mstari wa mbele hata hivyo aliuawa.
0 Comments