Ticker

7/recent/ticker-posts

CHOPA ILIYOPOTEA IRAN YAPATIKANA, RAIS EBRAHIM NA ABIRIA WOTE WAMEFARIKI DUNIA

Rais wa Iran, Ebrahim Raisi
IRAN

Chopa iliyombeba Rais wa Iran Ebrahim Raisi, Waziri wa Mambo ya Nje Hossein Amir-Abdollahian na maofisa kadhaa wa serikali ya Iran imepatikana huku ikielezwa kuwa watu wote waliokuwa ndani ya chombo hicho cha usafiri wamefariki dunia

Ajali ya kupotea na baadae kuthibitishwa kuanguka kwa chopa hiyo ilitokea Jumapili ya Mei 19,2024 Kaskazini-Magharibi mwa Iran. Usiku wa kuamkia leo Mei 20,2024 Chopa hiyo ilionekana katika maeneo hayo hayo ya Kaskazini-Magharibi mwa Iran kwenye mteremko wa kilima katika eneo la Varzaghan, karibu na mpaka wa Azerbaijan Mashariki.

 

Sehemu iliyopatikana Chopa hiyo

Mapema saa saba hadi nane zilizopita iliripotiwa kuwa ndege hiyo imepata ajali na wataalamu walianza kuisaka mara moja huku hali mbaya ya hewa ikitajwa kuwa ndio  chanzo cha ajali hiyo.

 

Ebrahim Raisi ameingia madarakani kuiongoza Iran mwaka 2021 na hiyo ni baada ya kugombea kiti cha urais mwaka 2017 na kushindwa. Mwanasiasa huyo mwenye umri wa miaka 63 kwa muda mrefu amekuwa akichukuliwa kama mrithi wa asili wa Kiongozi Mkuu Ayatollah Ali Khamenei.

 

Rais Ebrahim atakumbukwa zaidi kutokana na kuwa ni mwenye msimamo mkali na mwenye uhusiano mzuri na mahakama na wasomi wa kidini nchini humo.

 

Post a Comment

0 Comments