Ticker

7/recent/ticker-posts

BALILE AKABIDHIWA URAIS WA JUKWAA LA WAHARIRI AFRIKA MASHARIKI

 

Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), Deodatus Balile 

NA MWANDISHI WETU

Jumuiya ya Wahariri wa Afrika Mashariki (EAES), imemchagua Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), Deodatus Balile kuwa Rais wake kwa kipindi cha Mwaka mmoja 2024 - 2025.

 

Katika jukumu hilo Balile atasaidiwa na Makamu wa Rais, Fitihawok Yewondwossn, ambae ni Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Ethiopia.

Balile amechaguliwa baada ya kufanyika Mkutano Mkuu wa Jumuiya hiyo nchini Ghana, ikiwa ni baada ya kumalizika kwa Kongamano la Tatu la Vyombo vya Habari Afrika lililofanyika Accra, wiki hii.

 

Akizungumza kwenye mkutano huo baada ya kuchaguliwa kuwa rais, Balile alisisitiza umuhimu wa kupata taarifa kama haki ya msingi inayowezesha kupatikana kwa haki nyingine.

Alielezea umuhimu wa EAES kuhakikisha haki hiyo inapatikana na kufurahiwa na raia wote wa Afrika Mashariki na kwingineko.

 

Pia alisisitiza haja ya ushirikiano kati ya vyombo vya habari na serikali, vyama vya siasa, jumuiya za kiraia, na jumuiya za kimataifa.

Jumuiya hiyo inaundwa na nchi ambazo ni Kenya, Uganda, Tanzania, na Ethiopia, ambapo nchi zote wanachama zilishiriki uchaguzi huo.

 

 

Post a Comment

0 Comments