Afisa Mifugo wilaya ya Handeni mkoani Tanga, amefariki dunia baada ya kumgonga bundi na pikipiki aliyokuwa akiiendesha yenye namba za usajili STM 0232.
Ajali hiyo imetokea asubuhi ya leo Mei 17,2024 katika eneo la Sindeni jirani na kona ya PRS2.
Walioshuhudia ajali hiyo wanasema kuwa baada ya afisa mifugo huyo kumgonga bundi alipoteza mwelekeo hali iliyosababisha pikipiki yake kuyumba na kuanguka, mtaalamu huyo wa mifugo alipasuka kichwa na bundi alikufa papo hapo.
0 Comments