Ticker

7/recent/ticker-posts

SERIKALI YAIPA KIPAUMBELE AGENDA YA USALAMA WA CHAKULA

NA VICTOR MAKINDA: MOROGORO... 
SERIKALI imeipa nafasi kubwa ajenda ya usalama wa chakula ikizingatia dira ya kujilisha na kuwalisha wengine kibiashara na kuhakikisha mipaka ya nchi inakuwa wazi kwa kuuza chakula nje ikiwa ni sehemu ya kukamilisha mipango sita ya SDG iliyowekwa ikiwemo kukomesha baa la njaa nchini hadi kufikia mwaka 2030. 
Mkurugenzi wa masoko na usalama wa chakula kutoka Wizara ya Kilimo Gungu Mibavu alisema hayo jana kwenye mkutano wa wadau wa masuala ya usalama wa chakula (National Food system pathways roadmap and costed action plan) ulioandaliwa na Shirika la kilimo na chakula (FAO) (Food and Agricultural Organization of the United Nations) na kufadhiliwa na UN cordination food system na kufanyika mjini hapa. 
Alisema mpaka sasa chakula kilichopo kinatosheleza nchi na kubakiwa na ziada na kwamba hiyo inaonesha ni njia ya sahihi ya kufikia malengo ya milenia yaliyokusudiwa. Aidha Mibavu aliwataka wadau wa mkutano huo kujidhatiti na kuhakikisha wanatumia vizuri miaka sita iliyobakia ya kukamilisha malengo endelevu ya Maendeleo ya Milenia (SDG) ya mwaka 2030 waliyojiwekea tangu mwaka 2021.

Alisema tayari wameshasaini itifaki mbalimbali ikiwemo protocal ya SADEC, EAC inayohusu biashara na African treated area ambapo utekelezaji wa dira ya kujilisha wenyewe na kuwalisha wengine kibiashara upo katika kuongeza uzalishaji wa ndani wa chakula kuanzia kwenye kata zilizopo. 

Naye Mratibu wa uhimilivu wa mifumo ya chakula kutoka Zanzibar Sihaba Vuai alisema katika kuhakikisha wanafanya mageuzi ya kilimo wamejikita kwenye mifumo ya minyororo ya thamani 6 iliyopo kwenye mazao ya kipaumbele.
 
Vuai ambaye pia ni Mkurugenzi msadizi wa masuala ya sera aliyataja mazao hayo ya kipaumbele kuwa ni pamoja na mazao ya kilimo, matunda, viungo, mifugo na mengine sambamba na kujikita katika kuimarisha miundombinu ya uzalishaji katika kilimo cha umwagiliaji wa mpunga na mazao ya mbogamboga. 
Aidha alisema Serikali kwa sasa ina mpango wa kushirikisha serikali za mitaa katika masuala ya kilimo na kuwezesha wilaya 10 kati ya 11 zilizopo Zanzibar kunufaika zaidi na kilimo badala ya kutegemea serikali pekee. 

Alisema kwa sasa Wizara itasimamia utekelezaji wa sera, uwekaji wa mikakati na utekelezaji wake utafanywa na kila serikali ya mtaa kwa kuwa na wataalamu huku ikisimamia wakulima kwa kuhifadhi maeneo ya kilimo na kuleta ushirikishaji katika kutatua tatizo lolote litakalojitokeza kwenye kilimo biashara.

Post a Comment

0 Comments