Ticker

7/recent/ticker-posts

RAIS SAMIA, MUSEVENI WAWEKA DOLA LAKI NNE KWENYE MASHINDANO YA CECAFA

Rais Samia Suluhu Hassan wa Tanzania na Yoweri Museveni wa Uganda wamedhamiria kuliboresha soka la akanda wa Afrika Mashariki kwa kuamua  kudhamini Michuano inayosimamiwa na Baraza la Vyama vya Soka kwa nchi za Afrika Mashariki na Kati ‘CECAFA’.

Museveni ametoa Dola za Marekani 300,000 ambazo amezielekeza kudhamini mashindano ya Chalenji upande wa wanaume huku Rais Samia akitoa Dola 100,000 kudhamini Michuano ya timu za soka za taifa za wanawake kwenye ukanda wa ‘CECAFA’.

Taarifa hiyo imetolewa na Rais wa Baraza la Vyama vya Soka kwa nchi za Afrika Mashariki na Kati ‘CECAFA’ Wallace Karia jijini Dar es salaam alipokuwa akifanya mahojiano maalum na redio ya EFM.

Amesema awali Rais Samia alitoa kiasi hicho cha fedha kudhamini Ligi ya Mabingwa ukanda wa ‘CECAFA’ lakini kuepusha mgongano wa kimaslahi na wadhamini wa Shirikisho la Soka la Afrika ‘CAF’ kampuni ya Total Energy wameamua kupeleka fedha hizo kudhamini timu za soka za taifa za Wanawake ukanda wa Afrika Mashariki na Kati.

"Mkutano Mkuu umeamua kuhamisha zawadi ya Rais Samia ya Dola 100,000 kwenda kudhamini mashindano ya timu za taifa za wanawake kuepusha mgongano wa kimaslahi na Shirikisho la Soka Afrika ‘CAF’ na kampuni ya Total Energy inayodhamini Ligi ya Mabingwa Afrika," amesema Karia.




Post a Comment

0 Comments