Ticker

7/recent/ticker-posts

SOKA LA AFRIKA SASA LIMEHAMIA MOROCCO

NA ELIAS SHADRACK

Michuano ya kuwania kombe la Mataifa Afrika -AFCON kwa msimu wa mwaka 2023/24 yamekamilika kwa kishindo. Shirikisho la Soka Afrika (CAF) lilifanikiwa kuileta dunia Afrika kutazama fainali hizo zilizofanyika nchini Ivory Coast.

Inakadiriwa zaidi ya watu bilioni mbili walikaa mbele ya runninga zao na kuangalia michezo ya AFCON kutoka ngazi ya makundi mpaka fainali.

 

Nchi mwenyeji wa fainali hizo ndio imekuwa bingwa katika msimu huu baada ya ushindi wa goli 2-1 walioupata dhidi ya timu ya taifa ya Nigeria.

 

Ukweli ni kwamba mwisho wa safari moja ndio mwanzo wa safari nyingine ya mchuano hii ya Afcon ambapo baada ya Ivory Coast, AFCON nyengine inatarajiwa kufanyika nchini Morocco 2025 na baadae mwaka 2027 itafanyika katika mataifa ya Africa mashariki (Tanzainia, Kenya na Uganda) 

 

Katika michuano ya Afcon iliyomalizika changamoto zilizo kuwa zikilalamikiwa ni pamoja na ununaaji wa tiketi na miundombinu mibovu ya kufika uwanjani.

 

Kwenye hili la uuzwaji wa tiketi ni jukumu la CAF, kutengeneza mifumo sahihi ya kununua tiketi katika michuano ijayo ili changamoto iliyojitokeza Ivory Coast ya watu kukosa tiketi kwa madai kuwa zimekwisha zisijirudia tena na hili la miundombinu ni jukumu la muandaji wa michuano kutengeneza miundombinu rafiki kwa timu na mashabiki kufika uwanjani kwa wakati.

 

Kuhusu suala la waamuzi, CAF ilifanikiwa kuteua waamuzi sahihi wenye uwezo mkubwa wa kutafsiri sheria za soka pamoja na matumizi ya teknolojia ya video (VAR), hivyo kupunguza malalamiko.

 

Katika Afcon inayotarajiwa kufanyika Afrika mashariki mwaka  2027, Tanzania ina nafasi kubwa ya kufanya vizuri kutoka na sababu za kijeografia na hamasa kubwa kutoka kwa mashabiki wake. 

Tunapaswa kukubali kuwa sasa Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF) linapaswa kuiandaa timu mapema na kufanya ushirikiano na waandaaji wenza (Kenya na Uganda) ili kuhakikisha michuano inaandaliwa vizuri na timu ya Taifa inatoa changomoto katika michuano hiyo kama walivyofanya Ivory Coast.

Post a Comment

0 Comments