Ticker

7/recent/ticker-posts

SERIKALI YAWATAKA WAANDISHI KUANDIKA HABARI ZA MALIASILI ZENYE TIJA KWA TAIFA

 

Mkuu wa Kitengo cha Mawailiano cha Wizara ya Maliasili na Utalii, John Mapepele.

NA. JOHN I BERA- BAGAMOYO. 
Serikali kupitia Wizara ya Maliasili na Utalii imetoa rai kwa Waandishi wa Habari za Mazingira nchini ambao pia ni wanachama wa Chama cha Waandishi wa Habari za Mazingira (JET) kuhakikisha wanaandika habari za maliasili zetu zitakazoleta tija kwa taifa.

Rai hiyo imetolewa Februari 22, 2024 na Mkuu wa Kitengo cha Mawailiano cha Wizara ya Maliasili na Utalii, John Mapepele alipokuwa akifungua mafunzo ya siku mbili ya waandishi wa habari yaliyoaandaliwa na  JET kwa ufadhili wa Mradi wa Kupunguza Migogoro Baina ya Binadamu na Wanyamapori Tanzania, unaotekelezwa na Shirika la Maendeleo la Ujerumani (GIZ) kwa 
niaba ya Serikali ya Ujerumani (BMZ).

 Katika mafunzi hayo Serikali imewataka waandishi hao  kuzingatia weledi katika kuelimisha jamii hasa katika utoaji wa taarifa zinazohusiana na migongano  baina ya Binadamu na Wanyamapori ili ziweze kuwasaidia  waandishi hao waweze kutoa taarifa sahihi ambazo zitasaidia Taifa katika suala zima la  uhifadhi.

 

Mradi huo unahusisha mikoa ya Ruvuma na Lindi na wilaya husika ni tatu ambazo ni Liwale (mkoani Lindi), Namtumbo na Tunduru (mkoani Ruvuma).

Mapepele amesema kwa sasa wizara ina falsafa mbili kubwa  ambazo ni uhifadhi  na Utangazaji utalii  na hivyo mafunzo hayo lengo lake kuu ni kusaidia katika  kuimarisha uhifadhi ili usaidie katika utangazaji Utalii suala mabalo ni muhimu kwa jamii na Taifa kwa ujumla

Washiriki wa mafunzo ya siku mbili wa Mradi wa Kupunguza Migangano baina ya Binadamu na Wanyamapori. 
"Uhifadhi ukiimarika mazao ya uhifadhi pia yataimarika kama vile utalii na hivyo kulifanya taifa kupata fedha za kigeni na kuimarisha uchumi wake kupitia hifadhi zetu." Alisema Mapepele.
Ameongeza kuwa, Wizara imewekeza nguvu kubwa katika njia bora na za kisasa kutangaza Utalii na kuhifadhi huku akimpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuimarisha uhifadhi ambapo amehakikisha uhifadhi unaendelezwa kwa ajili ya Vizazi vya sasa na vizazi vya baadae 

 

Aidha, Mapepele amewataka  wanahabari hao kutumia siku hizo mbili za mafunzo ambazo zitawasaidia wanahabari hao kujengewa uwezo kwa ajili ya kutoa habari za rasilimali zetu kwa faida ya Taifa kwa ujumla.



Post a Comment

0 Comments