Kabla ya michezo hiyo ya Februari 16, Yanga ambao ndio vinara wa Ligi Kuu walikuwa wamejikusanyia alama 40 ambazo ni mara mbili zaida ya alama walizokuwa nazo mzunguko wa kwanza katika msimu uliopita.
Pamoja na mambo mengine msimu huu umeoneka kuwa ni wa kitofauti kutokana na ushindani wa ubingwa kuhusisha timu tatu za Yanga, Simba na Azam, tofuti na ilivyozoeleka awali ambapo washindani zaidi ni Simba na Yanga.
Ni miezi mitatu tu sasa imesalia kwa Ligi Kuu msimu wa 2023/24 kukamilika hadi sasa ni ngumu kutabiri nani atakuwa bingwa.
Hadi kufikia mwishoni mwa mwezi Machi angalau wabashiri wa soka wanaweza kupata mwanga wan ani anaweza kuwa bingwa, ikumbukwe kuwa raundi ya pili ya ligi kuu iimeshaanza tangu Februari 17, 2024.
0 Comments