Kikosi cha Taifa Stasr |
Taarifa iliyotolewa na Shirikisho la Soka Barani Afrika ‘CAF’ imeeleza kuwa ni timu nane ambazo zitaanzia hatua ya awali ya mashindano ya kuwania kufuzu AFCON 2025 mwakani huku nyingine 44 ikiwemo Taifa Stars zikianzia moja kwa moja hatua ya makundi.
Timu nane ambazo zimepangwa kuanza hatua ya awali kuwania kufuzu AFCON 2025 ni Somalia, Djibouti, Sao Tome, Chad, Mauritius, Sudan Kusini, Liberia na Eswatini.
Sababu ya timu hizo kuanzia hatua ya awali ni kuwepo katika nafasi nane za mwisho za viwango vya ubora wa soka Afrika kwa mujibu wa chati iliyotolewa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Duniani ‘FIFA’ mwezi huu ambapo zitapangwa kukutana zenyewe kwa zenyewe kupata nne zitakazoungana na nyingine 44 ili kuwa 48 zitakazotengeneza makundi 12 yatakayotoa timu 24 zitakazofuzu.
Droo ya hatua hiyo ya awali ya kuwania kufuzu AFCON 2025, itachezeshwa leo Jumanne (Februari 20) Cairo, Misri kuanzia saa 8:00 usiku kwa muda wa Afrika Mashariki na mechi za hatua hiyo ya awali zitachezwa kati ya Machi 18 hadi 26 mwaka huu kwa mtindo wa mtoano wa mechi mbili za nyumbani na ugenini.
0 Comments