NA JIMMY KIANGO-AFRINEWSSWAHILI-DSM
Moja ya maeneo muhimu kwenye maisha ya wanyamapori ni mapito yao, ambayo kwa lugha ya pamoja yanaitwa shoroba.
Shoroba ni muhimu kwa uhai wa wanyamapori, hizo ndizo zinawasaidia kutoka eneo moja kwenda jengine kujitafutia malisho.
Pasipo na shoroba ni wazi idadi kubwa ya wanyamapori itatoweka duniani, ikumbukwe kuwa wanyama wanahama kutoka eneo moja kwenda jengine kwa umbali mrefu, kimsingi wanyama hawana mipaka.
Na maeneo pekee yanayowasaidia kujua wanakokwenda na kuweza kurudi walikotoka ni shoroba, kwenye njia zao wanajiwekea alama kadha wa kadha zinazowasaidia kutopoteza mwelekeo na ndio maana Tembo huwa hawasahau mapito yao hata awe amepita kwa miaka mingi nyuma.
Kwa kuzingatia umuhimu huo, Chama cha Waandishi wa Habari za Mazingira Tanzania (JET) kimeandaa mafunzo ya siku mbili kwa waandishi wa habari za Mazingira kutoka vyombo mbalimbali vya habari nchini yenye lengo la kuwapa elimu ya kuripoti kwa usahihi masuala ya uhifadhi wa wanyamapori na shoroba kwa ujumla.
Elimu hiyo italenga namna ya kupambana na Uharibifu wa Misitu na Kupambana na Uhalifu wa Wanyamapori, Mabadiliko ya Tabianchi na uhifadhi wa viumbe hai.
Mafunzo hayo yatajumuisha wanahabari 20 kutoka vyombo mbalimbali vya habari Tanzania Bara na Zanzibar na yanaanza leo Februari 15,2024 Wilayani Bagamoyo, mkoani Pwani.
Akizungumzia mafunzo hayo, Mkurugenzi wa JET, John Chikomo aliiambia AFRINEWSSWAHILI kuwa mafunzo hayo ni sehemu ya mradi wa USAID TUHIFADHI MALIASILI ambao unafadhiliwa na Shirika la Misaada la Marekani (USAID).
Mradi wa Tuhifadhi Maliasili ni wa miaka mitano na unalenga zaidi kushughulikia tishio la kutoweka kwa wanyama na viumbe hai nchini Tanzania.
“Kupitia mafunzo hayo, waandishi wa habari watajazwa maarifa, ujuzi na mtazamo sahihi wa kuripoti taarifa za uchunguzi kuhusu uhifadhi wa viumbe hai na masuala ya mabadiliko ya tabianchi.
Chikomo alisema wanahabari hao watajengewa uwezo kwenye eneo la uhifadhi wa shoroba ili kujua namna ya kuchunguza, kuripoti na kuchambua uhusiano wa wanyamapori, uhifadhi wa bahari na misitu, biashara haramu na ujangili na kukuza uhifadhi wa wanyamapori na masuala ya utalii.
Mbali na kutengeneza mitandao kwa kuwaunganisha waandishi wa habari na wadau wa uhifadhi katika ngazi tofauti pia waandishi wataboresha taarifa zao kwenye masuala ya shoroba.
Shoroba ya tatu ni Nyerere Selous-Udzungwa inayoungana na Hifadhi ya Taifa ya Milima ya Udzungwa iliyopo Ifakara mkoani Morogoro, shoroba ya Amani-Nilo inayounganisha maeneo ya asili ya Amani na misitu ya hifadhi ya nilo iliyopo wilayani muheza mkoani Tanga ni ya nne.
Shoroba ya tano ni ile ya Ruaha Rungwa -Katavi inayoungana na Hifadhi ya Ruaha, hifadhi ya Rungwa, Lukwati, hifadhi ya Pigi na Katavi iliyopo wilayani Chunya mkoani Mbeya.
Ruaha Rungwa-Inyonga ambayo inaungana na Hifadhi ya Taifa ya Ruaha, Rungwa na Inyonga zilizopowilaya ya Itigi na Sikonge katika mikoa ya Singida na Tabora ni shoroba ya sita na shoroba ya saba ni ile ya Mahale-Katavi inayoungana na Hifadhi ya Taifa ya Milima ya Mahale iliyopo wilaya ya Uvinza na Katavi iliyopo mkoani Kigoma.
0 Comments