Ticker

7/recent/ticker-posts

MALINYI WAFURAHIA 4R ZA RAIS SAMIA SULUHU HASSAN

 


 NA MWANDISHI WETU

 

Mkuu wa Wilaya ya Malinyi mkoani Morogoro, Sebastian Waryba amesema, uanzishwaji wa Baraza la Ardhi na Nyumba ni sehemu ya utekelezwaji wa 4R za Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika kukabiliana na migogoro.

 

Alitoa kauli hiyo wakati akizungumza na waumini wa madhehebu mbalimbali ya dini, taasisi za serikali, viongozi wa vyama vya siasa na wananchi walioalikwa katika Iftar ilitoandaliwa na ofisi yake kwa ushirikiano na Ofisi ya Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo.

 

“Iftari hii ni ishara ya mshikamano, umoja, upendo, maridhiano ambayo kiongozi wetu wa nchi anatamani hili liwepo mahala pote, na hii ndio 4R ambayo Rais anaipigania.

 

“Juhudi zimefanyika kuhakikisha baraza hili linaanza kufanya kazi kwa mara ya kwanza tangu wilaya yetu ya Malinyi ianzishwe mwaka 2016.

 

Nampongeza sana Mkurugenzi wa Halmashauri yetu ya Malinyi (Khamis Katimba) kwa kusimamia uanzishwaji wa baraza hili ,” alisema.

 


Akizungumza wakati wa Iftari hiyo, Katibu Tawala wa Malinyi, Saida Mhagama alisema, Malinyi inahitaji utulivu ili shughuli za maendeleo zifanyike.

 

“Bila kuwa na amani kwenye eneo letu hili, hakuna shughuli za maendeleo zinazoweza kufanyika, Baraza la Ardhi na Nyumba linaleta suluhisha ambao ilikuwa ikisubiriwa kwa muda mrefu.

 

“Wananchi walikuwa wakienda umbali mrefu kutafuta huduma ya namna hii, hakika walikuwa anaumia. 

 

Walikuwa wakienda mpaka Ulanga na Ifakara, lakini sasa huduma hii inapatikana hapa hapa,” alisema.

 

Mkurugenzi wa halmashauri hiyo Khamis Katimba alisema, migogoro ya ardhi imekuwa ikiadhiri pakubwa makusanyo ya mapato ya halmashauri.

 

“Kutokana na umuhimu wa baraza hilo, ofisi yetu (halmashauri) kwa kiwango kikubwa imetumia kulisukuma jambo hilo mpaka kuanza kazi.

 


“Tumeweza kutoa vitendea kazi na hata fedha kidogo kwa ajili ya kuhakikisha shughuli hizi zinaendelea kwa kuwa tunaamini, ni sehemu muhimu ya msingi wa amani na maridhiano hapa wilayani kwetu,” alisema.

 

Mkazi wa Malinyi, Emmanuel Senga alieleza kuishukuru serikali kwa kuanzia huduma hiyo ambayo itawasaidia wananchi katika kupunguza gharama za fedha na mudana.

 

“Hapo awali tulitumia gharama kubwa kwa kusafiri umbali mrefu kwenda Wilaya ya Ulanga na Wilaya ya Kilombero kwa ajili ya kupata huduma hii,” alisema.

 

Post a Comment

0 Comments