Ticker

7/recent/ticker-posts

MWAKA MMOJA TU NDIO UMESALIA KWA GORAN ERIKSSON KUISHI

"Sina maisha zaidi, nimesaliwa na siku 365 tu za kuendelea kuliona jua na mwezi, maisha yangu hapa duniani sasa yanahesabika."  Hiyo ni kauli ya aliyewahi kuwa Kocha Mkuu wa Timu ya taifa ya England ‘The Three Lions’ Sven-Goran Eriksson. 

 Eriksson ameweka wazi kuwa amebakisha mwaka mmoja wa kuishi baada ya kugundulika kuwa na saratani ambayo haiwezi kutibika. Kocha huyo mwenye umri wa miaka 75, ndie kocha wa kwanza wa kigeni kuinoa timu ya taifa ya England na aliiongoza nchi hiyo kufika Robo Fainali za Kombe la Dunia mwaka 2002 na 2006 na michuano ya Euro 2004.  
"Ukipata ujumbe kama huo, unalazimika kuithamini kila siku na unafurahi unapoamka asubuhi na unajihisi sawa, kwa hiyo ndicho ninachofanya," alisema Eriksson alipohojiwa na BBC World Sporting Witness. 

 Eriksson amefundisha soka kwa miaka 42, aligundulika kuwa na saratani mwaka mmoja uliopita hatua iliyomlazimu kuacha majukumu yake ya ukurugenzi wa michezo katika klabu ya Karistad ya Sweden miezi 11 iliyopita.
 Mbali ya kufundisha timu ya taifa, pia amefundisha Klabu za Degerfors na Gothenburg za Sweden, Benfica ya Ureno, AS Roma, Fiorentina, Sampdoria na Lazio za ltalia na ametwaa mataji kadhaa.

Post a Comment

0 Comments