Ticker

7/recent/ticker-posts

VAR YAIEPUSHIA KIPIGO MISRI MBELE YA MSUMBIJI AFCON

Marejeo ya kamera kwenye mchezo wa soka leo (VAR) Januari 14,2024 yamewasaidia Mabingwa wa kihistoria wa michuano ya AFCON timu ya Taifa ya Misri kuepuka kipigo mbele ya timu ya taifa ya Msumbiji. 

Mafarao wa Misri walilazimika kusubiri hadi katika dakika za nyongeza kusawazisha bao kwa mkwaju wa penati kupitia kwa nahodha waao Mohamed Salah. 

Bao la Salah liliisaidia timu hiyo kuondoka na alama moja baada ya kutoka sare ya 2-2 kwenye mchezo wa kundi B,  mwamuzi wa kati Dahane Beida alilazimika kuamuru mkwaju wa penati baada ya usaidizi kutoka kwa VAR baada ya mlinziwa time ya taifa ya Msumbiji,  Domingos Macandza kucheza madhambi wakati akipambana kuondoa mpira uliokuwa ndani ya eneo lao la hatari. Misri ni kati ya mataifa yanayopewa nafasi ya kutwaa ubingwa wa michuano hiyo.

Post a Comment

0 Comments