Mwanasoka wa kimataifa wa Brazili Mario Zagallo amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 92 huku akiwa anashikilia rekodi kadhaa kwenye ulimwengu wa soka duniani. Zagallo ambaye ndio binadamu wa kwanza kushinda kombe la Dunia kama mchezaji na kocha kwa nyakati tofauti alikuwa sehemu ya vikosi vya Brazil vilivyotwaa makombe yote matano ya Dunia yaliyochezwa mwaka 1958, 1962, 1970, 1994 na 2002.
Alianza safari ya kuchukua kombe la Dunia mwaka 1958 na 1962 kama mchezaji kisha mwaka 1970 alilichukua akiwa kocha mkuu, mwaka 1994 kama kocha msaidizi wa timu ya Taifa na mwaka 2002 akiwa mshauri wa kikosi cha Brazil.
0 Comments