Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA), Habibu Suluo ameagiza magari yote ya Kampuni ya Kilimanjaro Express kusitisha kutoa huduma ya kusafirisha abiria kuanzia Januari 8, 2024 kutokana na kukiuka mashariti ya leseni, ikiwamo kutotoa tiketi za kielektroniki na kuzidisha nauli kwa abiria, hadi pale Kampuni hiyo itakapofanya maboresha na kufuata Masharti ya Leseni yake. Akizungumza baada ukaguzi wa kushtukiza katika Stendi ya Magufuli pamoja na ofisi za Shekilango, Suluo amesema, leo Januari 6,2024 wamelikamata gari la kampuni hiyo linalofanya safari zake za (Dar-Moshi-Arusha) likiwa limezidisha nauli kwa abiria, kila abiria alilipishwa nauli tofauti.
"Tukawataka wawarejeshee nauli zao, wakakubali, lakini muda mfupi tumetoka kwenye ofisi zao wakakataa kurejesha, eti mpaka Bosi wao aseme, sasa tumewataka wasimame kusafirisha abiria hadi pale watakapojirekebisha."
0 Comments