Jeshi la Magereza limetoa jumla ya ekari 100 kutoka kwenye eneo lao lililopo Warret, Wilayani Hanang mkoani Manyara kwa ajili ya matumizi ya waathirika wa mafuriko ya Hanang yaliyotokea mwishini mwa mwaka jana. Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Geophrey Pinda ametembelea na kukagua eneo hilo lililotolewa na Jeshi la Magereza ambapo tayari eneo hilo limepimwa viwanja kwa ajili ya kuwahamisha waathirika wa mafuriko yaliyotokana na maporomoko ya mawe na matope kutoka mlima Hanang.
Pinda amefanya ukaguzi huo akiambatana na Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Queen Sendiga pamoja na viongozi wengine wa mkoa pamoja na wa wilaya ya Hanang.
Desemba 21, 2023 Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu), Jenister Mhagama alielekeza Wizara ya Ardhi kuhakikisha viwanja kwa ajili ya kuhamisha waarhirika maeneo ya Gendavi, Jorodom, Ganana na Katesh - Hanang vinapimwa na kukamilika kabla ya Desemba 31, 2023.
0 Comments