Ticker

7/recent/ticker-posts

MABADILIKO YA MTAALA WA ELIMU KUWASAIDIA VIJANA KUKITEGEMEA

MABORESHO YA MITAALA AMBAYO YANAENDA KUBADILISHA MFUMO WETU WA ELIMU 1. Mtihani wa darasa la saba utafutwa. Mwanafunzi akianza darasa la kwanza lazima amalize kidato cha nne. 

 2. Kutakuwa mtihani wa upimaji wa kitaifa wa darasa la sita (Standard Six National Assessment). 

 3. Mwanafunzi atatakiwa asome fani fulani kabla hajamaliza kidato Cha nne ili aweze kujiajiri au kuajiriwa baada ya kumaliza. 

 4. Lugha ya kufundishia na kujifunzia itakuwa kiswahili, Kiingereza kitakuwa Kama somo kwa shule za Kiswahili medium na lugha ya kufundishia English, kiswahili kitakuwa Kama somo kwa shule za English medium. 

 5. Elimu ya msingi itakuwa miaka 

6. Mwanafunzi ataanza darasa la kwanza akiwa na miaka 6, tofauti na ya sasa miaka 7. 

 7. Elimu ya awali mwanafunzi ataanza akiwa na miaka 5. 

 8. Masomo ya elimu ya msingi yatakuwa KKK, Jiografia, kiswahili, Sanaa na michezo, hisabati, sayansi, historia ya Tanzania na maadili, dini na kiingereza na stadi za kazi itachopekwa. 

 9. Kiingereza kitafundishwa kuanzia darasa la kwanza kwa shule za Kiswahili na kiswahili kitafundishwa kuanzia darasa la kwanza kwanza kwa shule za kiingereza. 

 10. Shule zenye uwezo zitafundisha walau somo moja la lugha za kigeni kama kichina au kifaransa. 

 11. Sekondari kutakuwa na mikondo 2, mkondo wa jumla na amali (ufundi). Mwanafunzi atachagua kutokana na uwezo, matakwa na malengo yake ya badae. 

 12. Mkondo wa amali (ufundi) utakuwa na fani za: -kilimo na ufugaji -umakenika -biashara na ujasiriamali -sanaa bunifu -elimu ya michezo -ufugaji wa nyuki -uchimbaji wa madini -urembo 

 13. Mwanafunzi wa mkondo wa amali atatakiwa kuchukua masomo manne (4) ya jumla na moja la fani. 

14. Masomo ya jumla la wanafunzi wa amali ni: -hisabati -elimu ya biashara -kiingereza -historia ya Tanzania na maadili 

 15. Wahitimu wa amali watapata vyeti viwili yaani: -cheti cha ujumla cha elimu ya sekondari (NECTA) -cheti cha amali (NACTVET) 

 16. Kila shule itakuwa na wakala wa VETA ili kusimamia maswala ya ufundi. 

 17. Kila shule haitakuwa na mikondo zaidi ya miwili ya ufundi, hii ni kwaajili ya ufanisi na fani ziwe zinaendana na fursa za eneo husika. 

 18. Kutaanzishwa somo jipya la mawasiliano ya kitaaluma (academic communication) katika A-level na ualimu. 

 19. Coding itafundishwa shule ya msingi. 

 20. Information and Computer Studies (ICS) itabadilishwa na kuitwa Computer Science. Somo limesukwa upya. 

 21. Civics itaunganishwa na historia ya Tanzania na maadili kwa O-level.

 22. O-level masomo ya lazima yatakuwa 6 badala 7 ya Sasa. 

 23. Katika O-level masomo ya Biology na Geography yatakuwa masomo ya kuchagua pia kwasababu maudhui yake yamekuwa kwenye masomo ya jiografia na sayansi ya shule ya msingi kwa mfano afya ya jamii, afya ya uzazi, magonjwa ambukizi nk. 

 24. Civics, maarifa ya jamii, uraia na maadili yamefutwa. Maudhui yake yameingia katika somo la historia ya Tanzania na maadili. 

 25. General Studies (GS) katika A-level itafutwa na maudhui yake yatawekwa katika somo la historia ya Tanzania na maadili na mawasiliano ya kitaaluma. 

 26. Kufuta baadhi ya masomo kumefanyika ili kuondoa tatizo la kujirudia rudia kwa maudhui. 

 27. Michepuo katika elimu ya O-level imeongezeka kutoka minne (4) hadi tisa (9). Michepuko iliyoongezeka ni: -sanaa -lugha -muziki -michezo -TEHAMA 

 28. Masomo ya O-level yatakuwa: -biology -physics -chemistry -history -geography -historia ya Tanzania na maadili -hisabati -kiswahili -english -elimu ya biashara -utunzaji wa taarifa za fedha -computer science -bible knowledge -elimu ya dini ya kiislamu etc 

 29. Astashahada ya ualimu itafutwa kisha itaanzishwa Stashahada (diploma) ya elimu ya awali, ualimu wa msingi na ualimu wa elimu maalumu. Watakaosoma Stashahada watakuwa waliomaliza kidato cha sita na itasomwa kwa miaka miwili. 

 30. Walimu wa sekondari wote watakuwa na Shahada (degree). Kwasababu nchi nyingi ndio wanaenda muelekeo huu. 

31. Vyuo vilivyokuwa vinatoa Stashahada (diploma) ya ualimu wa sekondari vitatumika kutoa continuous professional development.

Post a Comment

0 Comments