Kutokana na kufurahishwa na ushirikiano huo Mhandisi Ulanga ametoa zawadi ya kumaliza mwaka 2023 iliyokwenda sambamba na ujumbe maalum kutoka kwa afisa uhusiano wa shirika hilo, Bi. Adeline Berchimance na Bi. Rehema Nyangasa ambao wamemwakilisha Mkurugenzi huyo.
Wawakilishi hao pia wametoa salam kutoka kwa Kaimu Meneja Uhusiano wa Shirika hilo, Edwin Mashaz ambaye ameishukuru DCPC na kuiomba idumishe ushirikiano, vilevile ametoa rai kwa waandishi wa habari hususan wa klabu hiyo wanapopata changamoto yoyote kuhusu shirika wasisite kuwasiliana nae ili kupata ufumbuzi.
Kwa upande wake Katibu Mkuu wa DCPC Fatma Jalala ameishukuru TTCL na ameahidi kudumisha uhusianao huo haswa katika kuitangaza TTCL kupitia mitandao ya kijamii na kuwaonyesha watumiaji kuwa TTCL ndio Baba wa mawasiliano na wengie wanafuata, amesisitiza kuwa wote tunalengo moja la kuunga mkono juhudi za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan za kujenga nchi na kuwaletea wananchi maendeleo.
0 Comments