Ticker

7/recent/ticker-posts

DAWA ZA KULEVYA ZAIDI YA KILO 3000 ZAKAMATWA KIGAMBONI

Na Mwandishi wetu Zaidi ya Kilo 3,180 za dawa za kulevya aina ya Heroin na Methamphetamine zimekamatwa huko Kigamboni Jijini Dar es Salaam ikiwa ni kiwango kikubwa zaidi kihistoria kuwahi kukamatwa tangu kuanza kwa shughuli za udhibiti wa dawa za kulevya nchini. 

 Kukamatwa kwa dawa hizo zinazojumuisha kilo 2.180.2 za Methamphetamine na Kilo 1001.71 za Heroine kumefuatia operesheni maalum iliyoendeshwa katika Jiji la Dar es Salaam na Iringa ambapo kama dawa hizo zingeachiwa kuingia mtaani zingeathiri Watanzania Milioni 72 idadi ambayo ni kubwa ikilinganishwa na Watanzania Milioni 61.7 kwa mujibu wa sensa ya watu na makazi mwaka 2022.

 Kamishina Jenerali wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya DCEA, Aretas Lyimo amesema, operesheni hiyo imefanikiwa kuwakamata watu saba wakiwemo wawili wenye asili ya Asia na wengine watano ambao ni maarufu nchini.

Zaidi ya Kilo 3,180 za dawa za kulevya aina ya Heroin na Methamphetamine zimekamatwa huko Kigamboni Jijini Dar es Salaam ikiwa ni kiwango kikubwa zaidi kihistoria kuwahi kukamatwa tangu kuanza kwa shughuli za udhibiti wa dawa za kulevya nchini. 

 Kukamatwa kwa dawa hizo zinazojumuisha kilo 2.180.2 za Methamphetamine na Kilo 1001.71 za Heroine kumefuatia operesheni maalum iliyoendeshwa katika Jiji la Dar es Salaam na Iringa ambapo kama dawa hizo zingeachiwa kuingia mtaani zingeathiri Watanzania Milioni 72 idadi ambayo ni kubwa ikilinganishwa na Watanzania Milioni 61.7 kwa mujibu wa sensa ya watu na makazi mwaka 2022.

 Kamishina Jenerali wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya DCEA ARETAS LYIMO amesema, operesheni hiyo imefanikiwa kuwakamata watu saba wakiwemo wawili wenye asili ya Asia na wengine watano ambao ni maarufu nchini.

Post a Comment

0 Comments