Ticker

7/recent/ticker-posts

WATANZANIA WAZOA TUZO ZA ZIKOMO ZAMBIA

WATANZANIA wametikisa katika kinyang’anyiro cha tuzo za Kimataifa za Zikomo kwa kutwaa tuzo zaidi ya tatu kadhaa.

Tuzo hizo zilizotolewa usiku wa jana, mtangazaji Djaro Arungu ametwaa tuzo ya Mtangazaji bora wa Afrika mwaka 2023 na tuzo ya Mtangazaji mwenye ushawishi zaidi Afrika, pia imemtangaza Khalid Ali Gangana kuwa mshindi wa tuzo ya mtangazaji bora wa TV. Washindi wote wanatoka Shirika la Utangazaji Tanzania-TBC

Yericko Nyerere ametwaa tuzo ya Mwandishi bora wa vitabu.

Upande wa filamu pia umefanya vyema kupitia tamthilia ya Fungu langu kutwaa tuzo ya tamthilia bora Afrika chini ya mtayarishaji na muongozaji Jenifer Kyakya maarufu ‘Odama’. Pia Johari Chagula ametwaa tuzo ya Muigizaji bora wa kike.

“Asanteni sana Tanzania...nguvu yetu ni kubwa mnoo.Tuzo hii ni ya kwetu mashabiki zangu na wadau wote wa tasnia.” Amesema Odama.

Wakiwa nchini Zambia wawakilishi hao wa nchi, walipokelewa na kulakiwa na Balozi wa Tanzania nchini Zambia, Luteni Jenerali Mathew Mkingule.

Nyota hao wanatarajia kuanza safari ya kurejea nchini majira ya saa 8:55 mchana na kuwasili jijini Dar es Salaam saa 12:05 jioni.

“Tukutane Airport Dar mpokee tuzo yenu Watz kwa pamoja kama tulivyoipigia kura kwa kishindo.” Ameandika Yericko Nyerere


Post a Comment

0 Comments