Ticker

7/recent/ticker-posts

RAIS DKT.SAMIA ATUNUKU KAMISHENI KWA MAOFISA WAPYA WA JWTZ

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Dkt. Samia Suluhu Hassan leo Novemba 18,2023 amekagua gwaride la heshima kabla ya kutunuku  Kamisheni kwa Maafisa wanafunzi wa Kundi la 04/20-Shahada ya Sayansi ya Kijeshi na Kundi la 70/22 (Regular) kwa Cheo cha Luteni Usu katika sherehe zilizofanyika kwenye Chuo cha Mafunzo ya Kijeshi Monduli  (TMA) jijini, Arusha.

Akizungumzia suala hilo, Rais Dkt. Samia amesema anafarijika kuona jeshi letu likipiga hatua kubwa za maendeleo.

"Nafarijika kuona Jeshi letu likiendelea kupiga hatua kubwa za kimaendeleo na uwekezaji katika taaluma ya sayansi ya kijeshi na rasilimali watu. Weledi, nidhamu, uzalendo na hatua hizi za kuwa bora zaidi kwa faida ya taifa letu siku hadi siku tangu kuanzishwa kwake Septemba 1 mwaka 1964, ni faraja na fahari kubwa kwa nchi yetu."


Post a Comment

0 Comments